Imebainishwa kuwa ni asilimia kubwa ya watoto wa kike hawamalizi shule kutokana na kupewa mimba,kudanganywa na vitu vya thamani mbalimbali nakusababisa kutofikia malengo yao ya maisha.
Hayo yamebainishwa na muuguzi mkuu wa hospitali ya Mkoa wa manyara Theonestina Rwechungura wakati alipokuwa akiongea kwenye mjadala ulioandaliwa na mradi wa Je Nifanyeje? Unaofadhiriwa na watu wa USAID mjadala huo ulifanyika katika chuo cha ufundi cha St Joseph kilichopo maeneo ya Dareda Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani wa Manyara.
Alibainisha kuwa siku hizi si kama miaka ya nyuma kwa mtoto wa kike kumaliza shule au chuo kutokana na kuwa na tama,kudanganywa na vitu nakusababisha kukatishwa kwa masomo pamoja na kupata ujauzito.
Alisema kuwa mtoto wa kike anatakiwa kupatiwa elimu ya kutosha ili hapo baadaye aeweze kupambana na umaskini nasi kuwa tegemezi katika familia pamoja na jamii kwa ujumla.
Aliongeza kuwa ukimwi umekuwa wimbi kila sehemu wanazungumzia ukiwa shueleni,chuoni ili kuweza kutimiza malengo yao lazima wajiheshimu,kujitunza, kujiamini pamoja na kujithamini.
Aidha alisema kuwa ukiwa na tamaa utafanya vitendo viovu visivyofaa kwani tafiti za watoto wa kike wanakatishwa masomo kutokana na ujauzito hivyo wanatakiwa wajilinde ili kuweza kutimiza malengo yao.
Alisema kuwa wasichana wanatakiwa wajifunze kusema hapana na wajifunze kukataa bali waendelee na masomo yao wajieupushe na mambo ya vishawishi ndio chanzo cha vishawishi.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo kutoka ‘Je Nifanyeje Diana Nsindagi aliongeza kuwa mradi huo unalenga vijana hasa wa kike ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kiafya na kijamii amewataka watoto wa kike wasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za baadaye.
Pia alitaja mambo muhimu ya kuzingatia ili kuweza kufanya maamuzi sahihi ya kiafya na kijamii ni jiamini,jithamini,jitambue, jiheshimu,jiwekee malengo,tambua mila na desturi zinazokuzunguka,tambua jamii inayokuzunguka na imani yao.
Wakichangia mjadala huo washiriki hao ambao ni vijana wakike wamesema kuwa watoto wa kike wanatakiwa wawe na msimamo na maamuzi sahihi ili baadaye weweze kusonga mbele,wawe na mpenzi mmoja,wamshawishi mpenzi kupima afya,kutumia kondomu pia waepuke na makundi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment