Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 27, 2012

Meijo Laiza ametangaza kugombea nafasi ya Ujumbe Halmashauri Kuu ya CCM taifa...!

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro, bwana Meijo Laiza ametangaza kugombea nafasi ya Ujumbe Halmashauri Kuu ya CCM taifa(NEC) kupitia Wilaya ya Siha.

Akizungumza na Radio Kili fm katika zoezi la kuchukua fomu ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama, Laiza amesema kilichomsukuma kuchukua fomu kugombea nafasi ya juu ya kiuwakilishi ndani ya Chama ni kiu ya kutaka kurudisha imani ya wananchi kwa CCM na kuwasilisha sauti ya Vijana wa Siha katika Vikao muhimu vya chama.

Amesema kwa miaka mingi Wilaya ya Siha imekosa uwakilishi mzurio wa vijana katika vikao muhimu ya Chama na kutokana na kuwa kijana ameamua kuchukua fursa ya kuwawakilisha vijana wenzake.

Laiza amesema kuwa pamoja na Wananchi kumuomba kuwania nafasi za juu katika Chama, kwa muda mrefu kumekuwa na ulegevu katika kutekelezwa kwa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ahadi za Chama kitu ambacho kimechangia kwa Mkoa wa Kilimanjaro ambayo hapo zamani ilifahamika kuwa Ngome ya CCM kutekwa na Vyama vya Upinzani.

Wengine waliochukua fomu za kugombea nafasi ya UJumbe Halmashauri Kuu (NEC), ni Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Siha, Aggrey Mwanry na kada wa CCM Joha Mtawazo.

No comments:

Post a Comment