Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 29, 2012

Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Kutathmini zoezi la Sensa...!




 Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Saba cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini Dar es slaam.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania Dr. Herison Mwakiembe na Mh. January Makamba wakiendelea na Kikao chao cha saba cha Kamati hiyo katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini Dar es salaam.

 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania Mh.Sophia simba na Hajat Amina Mrisho wakifuatilia mijadala ya Kikao hicho kilichofanyika Mjini Dar es salaam.    

Kikao cha saba cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Nchini kimekutana leo mjini Dar es salaamu kutathmini zoezi la kuhesabu Watu lililoanza usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita ya Tarehe 26/8/2012. 

 Wajumbe wa Kikao hicho walikutana katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

 Akitoa Taarifa katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Albina Chuwa alisema hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya Watu waliokataa kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu naMakazi pamoja na uandikishaji wa Vitambulisho wa Uraia. 

 Dr. Alibina alisema Ofisi ya Takwimu ya Taifa ilizipatia Ofisi ya Polisi za Mikoa sheria na kanuni za Takwimu zinazoelezea kwa ufasaha haki za Mwananchi zinazompasa kujiandikisha kwenye zoezi la Sensa pamoja na zile zinazomkabili endapo atakataa kuhesabiwa. 

 Alisema hatua hiyo ililenga kurahisisha utekelezaji wa sheria hiyo ndani ya kipindi cha zoezi zima la kuhesabu Watu katika kipindi hichi cha Sensa ya Watu na Makazi yam aka 2012. 

 Kwa upande wao Mawaziri wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya Mapinduzi ya Zanzibar walisema jitihada zimechukuliwa katika kuipatia madodoso Mikoa ambayo ilikumbwa na upungufu wa Vifaa hivyo. 

 Walisema hatua hiyo ya haraka imefanywa ili kuona zoezi la hesabu ya watu na makazi na uandikishaji wa Vitambulisho vya uraia linamalizika kwa kwa mafanikio kama lilivyopangwa.

 Walifahamisha kwamba jumla ya shilingi Bilioni 22.8 awamu ya kwanza tayari zimeshapelekwa Mikoani kwa ajili ya wasimamizi na Makarani wa sensa na shilingi Bilioni 22.8 nyengine zitatolewa kabla ya Tarehe 30/8/2012. 

 Aidha walizielezea baadhi ya changamoto zilizojichomoza ndani ya zoezi hilo ikiwemo baadhi ya watu katika shehia miongoni mwa hizo ni pamoja na Chwaka,kilindi, Nungwi,Pangawe, Fundo, Kilwa na Lindi. 

Halkadhalika Mawaziri hao waliwanasihi Wananchi kwamba kila mwana Jamii anahakikisha anafanikisha zoezi zima la sensa ya Watu na Makazi Hapa Nchini. 

 Naye Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alivipongeza Vyombo vya Habari Nchini kwa juhudi ilivyochukuwa ya Kuhamasisha pamoja na kutoa Elimu kwa Umma juu ya umuhimu wa Sensa a Watu. 

 Balozi Seif alifahamisha kwamba ujumbe na Taaluma hiyo kwa kiasi kikubwa imewafikia Wananchi kwa asilimia kubwa kama ilivyotarajiwa. “ Waliokataa kuhesabiwa kwenye zoezi hilo la kuhesabu watu kwa kweli wana lao”. Alielezea Mwenyekiti huyo Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Nchini.

No comments:

Post a Comment