Kamati ndogo iliyoundwa na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu kupigania haki ya kufunguliwa kwa gazeti la MwanaHalisi, leo imeipa serikali siku saba kuliruhusu gazeti hilo kuendelea kuchapishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo Bwana Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya jambo hilo kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani.
Kamati hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia imeitaka serikali kutekeleza madai mbalimbali ikiwemo kulifungulia gazeti la Mwanahalisi maramoja.
Aidha kamati hiyo imeitaka serikali badala ya kushughulikia Watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu, ishughulike na wahalifu waliomteka Dkt. Stephen Ulimboka.
Gazeti la mwana halisi limefungiwa na Serikali kwa muda usiojulikana, kutokana na taarifa iliyotolewa na gazeti hilo toleo namba 304 kuhusu mawasiliano ya mwana usalama Ramadhani Ighondu, na namba zake za simu zote ambazo alikuwa akifanya mawasiliano na Dr. Ulimboka na watu mbali mbali.
No comments:
Post a Comment