Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 21, 2012

Maduka 40 ya dawa za Kilimo na Mifugo yafungwa kutokana na Makosa mbalimbali...!

Jumla ya Maduka ya dawa za kilimo na Mifugo 40 kutoka katika wilaya za Korogwe,Lushoto,Handeni na Kilindi yamefungwa  kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya kukosa vibali,kuuza dawa bandia,dawa zilizopitwa na wakati na kusababisha wakulima  na wafugaji  kupata hasara kubwa baada ya mazao na mifugo yao kuathiriwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Msajili wa viwatilifu nchini
Dr.Bakari Kaoneka  amesema taasisi hiyo  imeimarisha ukaguzi  nchini
kote baada ya kukithiri kwa udanganyifu kutoka kwa wafanyabiashara na kusababisha kero kubwa.

Amesema zoezi hilo ni la kudumu na litaendelea kwa mikoa mingine yote ili kuwabaini wauzaji wa dawa za mifugo na kilimo bandia na zile
zilizopitwa na wakati ili kuwanususru wakulima na wafugaji ambao wengi wao wamekuwa wakipata hasara baada ya kununua dawa hizo.

Amesema kuwa awali walikutana na upinzani mkubwa na kulazimika kutumia nguvu kuyafunga maduka hayo baada ya wafanyabiashara hao kukaidi amri
ya kufunga maduka yao baada ya kuwapatia amri ya kuyafunga.

Aidha wapo baadhi ya wafanyabiashara waliunga mkono zoezi hilo  kwa
madai kuwa ni kuleta uimara na ufanisi katika kupunguza hasara zisizo
za lazima kwa wakulima,wafugaji na hata wafanyabiashara wenyewe.

No comments:

Post a Comment