Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 21, 2012

Leo Mahakama Yatengua Ubunge Jimbo La Igunga...!


 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga akiondoka baada ya mahakama kutengua wake wa kiti cha ubunge.

Mahakama ya Tabora leo imetengua ushindi wa kiti cha Ubunge wa jimbo la Igunga, Tabora kilichokuwa kinakaliwa na Dkt. Peter Dalaly Kafumu (CCM).
Kesi dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mwalimu Joseph Kashindye.
Katika kesi hiyo Bwana Kashindye  amewashitaki Dkt. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi jimboni humo, Bw. Protace Mgayane.
Aidha imeelezwa kuwa  Bwana Kashindye amewashitaki kuwa wakati wa kampeni, watuhumiwa walitoa vitisho, ahadi ya ujenzi wa Daraja la Mbuntu na kugawa mahindi.
Akizungumza na waandishi wa habari hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Nzega, Bwana Silvester Kainda, amesema awali Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, ilipanga kutoa hukumu Agosti 20, mwaka huu lakini kwa bahati mbaya siku hiyo ilikuwa ni sikukuu hivyo ikaahirishwa hadi leo.

No comments:

Post a Comment