Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 21, 2012

Raia wa Uswisi auawa na Majambazi Dar...!
Fariji Msonsa na Mulemwa Mulemwa
RAIA mmoja wa Uswsi amekutwa amekufa nyumbani kwake maeneo ya Mbuyuni, Masaki.
Mtu huyo ambaye jina lake halikufahamika ni mwanaume mwenye umri kati ya miaka 30 hadi 35, alikuwa nchini kwa ajili ya utafiti katika Hospitali ya Mt Francis, Ifakara Morogoro.

 Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, siku ya tukio Ijumaa iliyopita, nyumba  jirani na alikokuwa anaishi marehemu, alivamiwa na majambazi wanane, mmoja akiwa amevaa sare za polisi.

 Kwa mujibu wa habari hizo, majambazi hayo yalimwamuru mkazi wa nyumba hiyo awakabidhi mali zake, alipowakabidhi waliondoka bila kumdhuru.
Baada ya tukio hilo mkazi huyo alikimbia kuomba msaada kwa jirani yake (sasa marehemu), lakini badala ya kupata msaada, yeye ndio akalazimika kuutoa kwa kuwa alimkuta sakafuni akiwa amefungwa kamba kikatilli.

Jirani huyo aliyeibiwa alilazimika kumpeleka hospitalini jirani yake, ambapo iligundulika kuwa alikuwa amefariki dunia kabla ya kufikishwa hapo.

Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa kifo hicho kinahusiana na tikio hilo la ujambazi. Hadi sasa Jeshi la Polisi halijafanikiwa kuwatia mbaroni majambazi hao, lakini linamshikilia mmoja wa walinzi wa eneo hilo kwa upelelezi zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela hakuweza kutoa majibu kamili juu ya tukio hilo akidai kuwa nje ya ofisi.

No comments:

Post a Comment