1. LAZIMA UJUE MADHARA YA KUJAMIIANA:Mimba ni suala la kwanza kulifikiria.Lakini kumbuka pia kuna magonjwa mengi sana yatokanayo na kufanya mapenzi kama zinaa na UKIMWI.
2. UWE NA NJIA MBADALA YA KUPAMBANA NA HAYO MADHARA: Ongea na mpenzi wako uone kama yuko tayari kutumia Kondom na Vidonge.Kamahayuko tayari,kuwa huru kufanya maamuzi sahihi.
3. MMEJIPANGA VIPI ENDAPO MTAPATA MIMBA?: Hata ungekuwa makini kivipi, ukweli nikwamba kondom nimuhimu sana hasa ikiwa hamko tayari kuwa wazazi kwa wakati huo .
4. HAKIKISHA UNA MIAKA 18 NAKUENDELEA: Kama hujafikisha miaka 18 nakushaur usithubutu kujihusisha na mambo ya mapenzi kwa sababu viungo vyako bado haviko tayari.Kujiingiiza katika mapenzi katika umri mdogo ni kujiharibia mfumo wako wa uzazi na kujijengea msingi wa kuwa tasa.Kumbuka sharia ziliwekwa makusudi ili zikusaidie wewe.
5.USIKUBALI KUFANYA MAAMUZI UKIWA UMELEWA.: Pombe haimuongozi mtu kufanya maamuzi sahihi.Epuka kufanya maamuzi yatakayo kufanya ujute maishani,tena kwa raha ya masaa machache tu..
6. MWAMINI MPENZI WAKO: Mimi naamini kuwa mpaka mtuunafikia hatua ya kumvulia mtu nguo ni kwamba una mwamini kweli kweli.Usikurupe.Tambua thamani ya mwili wako na kumbuka kuwa mapenzi hayalazimishi.Wengi waliolazimisha penzi waliishia kujuta na kujiua.
7. KUWA TAYARI KWA LOLOTE:Inawezekana kabisa ulichokuwa unakitegemea kwa mpenzi wako hukipati.Yawezekana akawa hajui mapenzi,si mbunifu au hakufikishi.Suluhu si kukimbia tatizo bali ni kutafuta jinsi ya kutatua .
Source: Mpekuzi
No comments:
Post a Comment