Zoezi la sensa ya watu na makazi kwenye mkoa wa Kigoma lilipata ugumu kutokana na waumini wa dini ya kiislamu wanaopinga kuhesabiwa kukimbilia misikitini hivyo kutofikiwa na makarani waandikishaji.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani Maneno amesema kwenye pitapita yao kufanya tathmini wamekutana na ugumu huo na tayari wameanza kuufanyia kazi, maeneo ambayo wamegundua tatizo hilo ni pamoja na Mwandiga na Katonga ambapo licha ya kutaka kuongea na viongozi wa misikiti hiyo, wameshindwa kupata ushirikiano wowote hivyo amesema kamati ya ulinzi na usalama inatarajia kukaa kujadili ili kuona hatua za kuchukua.
Amekaririwa akisema “kuna baadhi ya viongozi wa kiislam wameshawishi waislam wenzao kwenda kulala misikitini ili kusiwe na nafasi tena kwa makarani wa sensa kuingia misikitini, nilipojaribu kwenda kwenye msikiti wa Mwandiga kujaribu kushawishi niongee na viongozi wao, sikufanikiwa”
Mwandishi Fadhili Abdallah anasema Mkuu huyo wa wilaya amethibitisha jumla ya kaya 40 kati ya 64 kwenye kijiji cha Bubango kata ya Bitale Kigoma Vijijini, zimekataa kuandikishwa kufuatia maelekezo ya viongozi wa kaya
No comments:
Post a Comment