Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 3, 2012

Mastaa wa kike wamchinjia baharini Hemed a.k.a PHD...!

  

Hemed Suleiman a.k.a PHD

Hivi karibuni msanii wa filamu nchini, Hemed Suleiman a.k.a PHD alisikika kwenye vyombo vya habari mbalimbali na kuandikwa sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzua gumzo kwa kile alicho kitamka kwa mdomo wake wakati akihojiwa na Blog ya mvuto kwanza na kuulizwa idadi ya mastaa wa kike aliotembea nao ambapo alisema: “Unauliza kengele kanisani? Unadhani kwa nini naitwa Hemed PHD? Nina taaluma ya kucheza na mioyo ya mabinti hawa wa Kibongo ila tatizo hawanivutii, huwa napita tu. Mpaka sasa nishawapitia mastaa 32....” huku akijinadi kutotumia kondom wakati mwingine. 
Sakata hilo limechukua sura mpya baada ya baadhi ya mastaa wa kike tofauti tofauti wameeelezea kuwa wamekereka sana tena sana maneno hayo na kusema alichokifanya Hemed kimemchafua mbele ya jamii na kumshushia heshima sana, na hakuna mtu yeyote anayeweza kumsifia kwa kauli yake hiyo.

Aunt Ezekiel
“Akili zake si mzuri, kujisifia haimaanishi ni rijali kuliko wengine, ni upuuzi na ni hatari hasa ukichukulia kwamba kuna gonjwa la Ukimwi.”
Nisha
“Kusema hivyo atakuwa ameamua mwenyewe ila ametudhalilisha kwani ni bora kuwataja kuliko kuishia kutaja idadi kubwa, ila mimi simo.”
Thea
“Ni kukosa busara, anaonekana anatafuta umaarufu, tu bora angetaja hao aliotembea nao.”
Jack wa Chuz
“Hemed si taipu yangu kwa hiyo hata kwenye hiyo listi yake simo ila ningemuona mjanja kama angewataja.”
Jack Dustan
“Alichokifanya wala si kizuri, eti katembea na mastaa 32, ili iweje sasa? Atakuwa amekosa la kufanya ndo’ maana ....”
Rose Ndauka
“Kila mtu ana akili yake, siwezi kusema amekosea kutoa maneno hayo kwani akili yake ndiyo imemtuna na kila mtu ana maisha yake, ninachoshukuru mimi simo.”

No comments:

Post a Comment