Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 9, 2012

MAUNDA ZORRO: “SINA MPANGO WOWOTE WA KUFANYA MUZIKI AU KUTOA NGOMA MPYA KWA SASA” …!

WAKATI mashabiki mbalimbali wa muziki wakilalamikia wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya kutoa kazi chache nzuri pindi wanatoka na kupotea kwenye ramani, hali imejitokeza kwa Maunda Zorro ambaye aliigia kwenye tasnia hiyo kwa kasi na sasa yuko kimya muda mrefu huku akidai kuwa hana mpango wowote wa kufanya muziki au kutoa ngoma mpya kwa sasa.
Maunda Zorro aliongea na mwandishi wa DarTalk, baada ya kuulizwa vipi tangu mwaka huu ulipoanza hakuna kazi yoyote aliyoitoa zaidi kushirikishwa, ambapo alijibu kuwa hana mpango wowote wa kutoa wimbo na wala kurejea kwenye muziki.
Maunda katika pozi

Kauli hiyo ya Maunda haikuwa ya upole kwani alionekana kujibu kwa ukali na mwandishi wa habari hizi alipojaribu kujua ni kitu gani kinachomfanya asifanye ngoma mpya au kurejea kwenye muziki, hakujibu zaidi kudai kuwa hana cha kuzungumza juu ya ishu hiyo.
“Kaka mbona hunielewi mimi nimekuambia sina chochote kwa sasa tena sina mpango wowote, mbona unaendelea kuniuliza maswali ambayo majibu yake sina, nachokuambia ni kwamba sina mpango wowote kwa sasa,”
alijibu Maunda kwa ukali.
Mwandishi alipojaribu kutaka kujua nini sababu hasa haikuweza kupata jibu, lakini tetesi zinasikika mtaani kuwa mwanaume aliyezaa na msanii huyo ndiye anayeweka pingamizi juu ya mwanadada huyo kufanya muziki.

No comments:

Post a Comment