THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia
Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Fatma Abubakar Mwasa kufuatia
taarifa za vifo vya watu 17 wakiwemo watoto watano vilivyosababishwa na ajali
ya Basi la Kampuni ya Sabena iliyotokea katika eneo la Kitunda, Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora siku ya
Jumanne tarehe 7 Agosti, 2012.
“Nimesikitishwa
na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za vifo vya watu 17 waliofariki papo
hapo baada ya Basi la Abiria la Kampuni ya Sabena kupata ajali katika eneo la
Kitunda Wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora”, amesema Rais
Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi na kuongeza,
“Kwa mara
nyingine tena tunashuhudia kupotea kwa maisha ya ndugu zetu 17 wasiokuwa na
hatia kutokana na ajali za barabarani za mara kwa mara ambazo busara na hekima
ya madereva na uwajibikaji wa pamoja wa vyombo vyenye dhamana na usimamizi wa
Sheria ya Usalama Barabarani vinahitajika sana kuepusha vifo vya aina hii”.
“Kwa dhati ya
moyo wangu, ninakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Fatma Mwasa
Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kutokana na msiba huo mkubwa
uliotokea Mkoani kwako. Aidha naomba
unifikishie rambirambi hizi kwa ndugu na jamaa wa watu wote waliofikwa na msiba
huu. Nawaomba wote wawe na moyo wa
uvumilivu na subira wakati huu wa kuomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao. Ninawahakikishia
kuwa niko pamoja nao katika maombolezo haya”, ameongeza
kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Amesema
anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azilaze mahala pema peponi roho za
Marehemu wote, na awawezesha kupona haraka majeruhi 78 wa ajali hiyo, ili
warejee katika hali ya kawaida na
kuungana tena na ndugu na jamaa zao.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
9 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment