Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 4, 2012

MTOTO AOKOTWA PPF TOWER ALAZWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI...!


Mtoto mdogo mwenye kati ya mwaka mmoja au miaka miwili amekutwa eneo la PPF Tower, Jijini Dar Es Salaam leo saa sita mchana. Amekutwa na wasamaria wema akiwa amelala chini eneo hilo.
Wasamaria wema hao waliamua kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na Askari wa Central Police. 
 Yeyote mwenye taarifa juu ya mtoto huyo au anayeweza kumtambua kwenye picha hiyo hapo juu anaweza kuwapa taarifa wazazi wa mtoto huyu au kutoa taarifa kwenye kituo chochote cha polisi kilichopo karibu, au unaweza kupiga namba 0755 64 86 36 au 0715 64 86 36 ili kuweza kufanikisha zoezi la kumkutanisha mtoto huyu na wazazi wake.

Mtoto huyu bado yupo Hospitalini ya muhimbili anaendelea kuhudumiwa. 
Tafadhali sambaza ujumbe huu ili kufanikisha zoezi hili.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili

No comments:

Post a Comment