Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 31, 2012

Mwanafunzi wa shule ya msingi afariki dunia baada ya kushika Mota...!

MWANAFUNZI wa shule ya msingi  Mkapa, Matayo John (9) iliyopo  wilayani
same mkoani kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kushika mota
iliyokuwa  imewashwa
kwa ajili ya kupandisha  maji ya kisima.

Kamanda  wa polisi mkoani hapa Robert Boaz, amethibitisha  kutokea kwa
tukio hilo na kwamba lilitokea august 29 mwaka huu majira ya 11:30 wilayani
humo wakati mtoto huyo akicheza na wenzake.

Kamanda alisema mtoto huyo aligusa mita ya kupandishia maji ya kimasima
ambayo ilikuwa imewashwa na kufariki kwa kupigwa shoti ya umeme.

Boaz alisema mota hiyo ilikuwa nyumbani kwa Rajabu Abdala ambapo marehemu
huyo alikuwa akicheza maeneo hayo akiwa na wanzake.

Kamanda amewataka wazazi na walezi kuangalia watoto wao wakati wanatumia
vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao ili kuweza kuepusha vifo visivyo
vya lazima kwa watoto.

No comments:

Post a Comment