Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 29, 2012

RAIS AAGIZA BUNGE LIFUTWE...!

Mafuriko Senegal 
 
Rais wa Senegal, Macky Sall ametoa wito wa kufutiliwa mbali bunge la Senate, huku pesa ambazo hutumika kulipia shughuli za bunge hilo zikitumika kwa msaada wa chakula.
Rais huyo alikatiza ziara yake nchini Afrika Kusini kuweza kushughulikia mafuriko makubwa yanayokumba nchi hiyo na ambayo yamesababisha vifo vya watu 13.
Akiongea akiwa katika uwanja wa ndege wa Dakar rais Macky Sall, alisema kuwa ataweza kuwasilisha mswaada wa dharura bungeni ili kufutilia mbali bunge la Senate.

Pesa ambazo hutengewa shughuli za bunge hilo, ambazo ni takriban dola milioni 15, zitaweza kutumika kuzuia mafuriko zaidi katika siku za usoni.

Ingawa maeneo ya nyanda za chini nchini Dakar hukumbwa na mafuriko kila msimu wa mvua, mwaka huu athari zimekuwa kubwa kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi. .

Inakisiwa maelfu ya watu wameachwa bila makao.

Hapo awali, wananchi walifanya maandamano kutuhumu serikali kwa kukosa kuchukua hatua mwafaka kukabiliana vilivyo na hali hiyo ya mafuriko ingawa walitawanywa na gesi ya kutoa machozi.

Rais Sall alielezea umuhimu wa bunge la Senate katika mfumo wa demokrasia lakini akasema kuwa afueni ya watu wanaoathirika kutokana kwa mafuriko hayo ni muhimu kuliko bunge hilo.

Mwezi Mei mwaka huu, benki ya dunia iliahidi kutoa dola milioni 55.6 kuweza kuimarisha miundo mbinu itakayowezesha nchi hiyo kukabiliana na mafuriko.

Nchi hiyo imekuwa mfano mzuri wa nchi yenye demokrasia barani afrika ikiwa na mfumo mzuri wa siasa za vyama vingi na mfumo wa majimbo.

chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment