Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 16, 2012

Rais Yoweri Museveni wa Uganda Aunda Tume ya Kuchunguza Chanzo cha Kuanguka kwa Helkopta Tatu za Jeshi...!

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amebuni jopo maalumu litakalochunguza
kisa cha kuanguka kwa helkopta 3 za jeshi la nchi yake huko nchini Kenya
siku ya Jumapili.

Jopo hilo litakaloongozwa na aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Uganda
Jenerali Salim Saleh linatarajiwa kutafiti chanzo cha ajali hiyo ambapo
wanajeshi wawili wamethibitishwa kufariki dunia.

Wakati huo huo Rais Mwai Kibaki ametuma risala za rambirambi kwa Rais
Museveni ambapo pia amemuahidi kwamba serikali ya Kenya itashirikiana
na jopo hilo ili kupata ukweli wa chanzo cha mkasa huo.

Mapema jana, mabaki ya Helikopta mbili za Jeshi la Uganda zilizokuwa
zimeripotiwa kutoweka yalipatikana katika msitu wa mlima Kenya.
Wanajeshi wawili wa Uganda wamethibitishwa kufariki dunia huku wengine
wanne wakiwa bado hawajulikani walipo.

Jumla ya wanajeshi 15 wa UPDF waliokuwa kwenye helikopta hizo
wameokolewa.

No comments:

Post a Comment