Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 16, 2012

Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) mkoani Kilimanjaro limekana kuhusika na usambazaji wa vipeperushi vinavyoshawishi wananchi kususia zoezi la Sensa...!

Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) mkoani Kilimanjaro limekana kuhusika
juu ya vipeperushi vinavyosambazwa kushawishi watu wasishiriki katika
sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia
augusti 26 mwaka huu.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha baraza hilo,shekhe mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Sheikhe Shaban Rashid amesema wao kama baraza
hawahusiki na vipeperushi hivyo na kwa yeyote anayehusika yafaa
kuchukuliwa hatua kali.

Sheikhe Shaban ameyasema hayo baada ya kukamatwa kwa watu sita
wilayani mwanga na wilayani same ambapo amesema kitendo cha
kusambaza vipeperushi hivyo kwa dini ya kiislamu ni aibu kwani ni kuipinga
serikali kwa kutotii maagizo yake ambayo ni kwa manufaa ya wananchi
wake na waislamu pia.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo sheikhe Ramadhan Salim
amewataka waislamu mkoani hapa kuwapuuza wanaosambaza vipeperushi
hivyo na kuunga mkono jitihada za serikali ili kufanikisha zoezi hilo
ambalo ni kwa manufaa ya taifa zima na waislamu kwa ujumla sanjari na
kuwaonya wale wanaotaka kugomea zoezi hilo kutokufanya hivyo kwani ni
kinyume na taratibu za dini ya kiislamu.

No comments:

Post a Comment