Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 1, 2012

SHILOLE: MATAPELI WANAVYOTAJIRIKA KUPITIA JINA LANGU...!


Zuwena Mohammed ‘Shilole’  alisema kuwa kuna mtu/watu wamekuwa wakitumia jina lake kwenye mtandao wa Kijamii wa Facebook na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki zake wamtumie fedha kwa kuwa mwanaye ni mgonjwa sana na anatakiwa kupelekwa India kwa matibabu, Shilole amekanusha usemi huo na kusema hao ni matapeli wanataka kujipatia pesa kupitia jina lake.. Wakati habari hizo hazina ukweli wowote.
“Jamani huyu mtu ni Shilole feki, tena ananidhalilisha sana kwa kuonesha kuwa nina matatizo wakati si kweli, kama ningekuwa na matatizo ningetumia magazeti na mitandao ingefuata baadaye,” alisema Shilole.
Staa huyo anayetamba na muziki wa mduara alisema kuwa aligundua hila hiyo baada ya kukutana na mtu barabarani na kumpa pole kwa kuuguza mtoto wake na kumuuliza kama alipata michango aliyoiomba kupitia Facebook.

“Natoa taadhari kwa mashabiki wangu wasikubali kumchangia mtu huyo kwani ni tapeli anayetumia jina langu kujipatia kipato, siku nikiwa na matatizo watayajua kupitia magazeti,” alimalizia kwa kusema hivyo.
 

No comments:

Post a Comment