Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 2, 2012

UTAPELI WA AJABU WAIBUKA DAR ES SALAM…!


Kwa wakazi wa Dar es salaam na waliopo mikoani hii ndio njia wanayoItumia matapeli kujipatia mali. Utapeli huu ulianza kama utani takribani miezi mitatu iliyopita na ulianza kama utani lakini kwa sasa umezidi kupamba moto hasa kwa wakazi wa Dar es Salaak na hususani kwa wanawake. Na mpaka sasa wanawake zaidi ya wane wamesha  report kuhusu kutapeliwa kwa njia hii ya kupigiwa simu au kufuatwa katika eneo lako la kazi na watu wasio wajua na kujitambulisha kwao na kuwaeleza mambo mengi yahusuyo biashara na katika kuhakikisha kuwa wanafanikisha utapeli wao husema wameagizwa na ndugu, jamaa au rafiki yako wa karibu ambaye wanauhakika unamjua na baada ya hapo huanza kukuelekeza sehemu ya kwenda kukutana au kumsubiri rafiki yako huyo walio kutajia huku wakijitahidi kukupumbaza akili ili usiweze kumpigia simu.. Wakishafika hotelini au kwenye mgahawa hukupa fursa ya kuagiza kinywaji na hapo ndipo wanapofanikisha adhma yao maana kwenye kinywaji utakacho kiagiza wenyewe hukiwekea madawa ya kulevywa, unapomaliza kinywaji papo hapo unapoteza fahamu na matapeli hao huchukua kila ulichonacho na kukupeleka mpaka karibu na nyumbani kwako na kukutelekeza na unapopelekwa hospitali na kupata matibabu na kurudi kwenye hali ya kawaida unapompigia mtu uliyetajiwa na matapeli wale kuwa kuna biashara mnakuja kuifanya mtu huyo hushangaa na kukana kuwafahamu matapeli hao…

ANGALIZO: Ni vyema kwa yeyote atakaye pata ujumbe huu amfahamishe na mwenzake ili kumuepusha na matapeli hawa ambao kwa sasa wamezidi kuwa wajanja sana.

No comments:

Post a Comment