Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 30, 2012

SIRI NZITO KUHUSU DIAMOND NA MAMA YAKE...!

SIRI imefichuka! Kumbe mwanamuziki ‘anaye-hit’ kwa sasa katika muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platinumz’ na mama yake mzazi, Sanura Khassim ‘Sandra’ walianza kupendana zamani, 

Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya familia hiyo, Sandra ndiye aliyemlea Diamond na kupita katika vipindi vigumu kimaisha baada ya baba yake, Abdul Jumaa kutengana na mama yake ndiyo maana mara nyingi huwa wanaambatana hata kwenye show za msanii huyo ambazo kuna uwezekano wa mzazi huyo kuhudhuria.

“Sandra ndiye aliyemsomesha Diamond kwa shida hivyo hawezi kuacha kumpenda na ndiyo maana kila sehemu akiambiwa awashukuru watu waliomfikisha hapo alipo, huwa mtu wa kwanza kumtaja ni mama yake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Wewe msikilize Diamond, huwa anaanza kumshukuru Mungu ‘then’ anafuatia mama yake.”
Chanzo hicho kilitiririka kuwa kuna wakati Diamond hata anasahau suala la kuoa kwa sababu anapata upendo wa kutosha kwa mama yake. Hata mama yake naye ndiyo maana hawezi kuolewa kwa sababu tayari kuna mtu wa kumfariji ambaye ana upendo wa dhati kwake. Sasa maisha yanataka nini tena?

Kwa mujibu wa Diamond mwenyewe, wakati anaanza kuhangaika kuchomoka kimuziki, mama yake alikuwa akimpeleka kwenye ‘talent show’ hivyo mafanikio yake ni dhahiri kuwa yeye ndiyo mwenye mchango mkubwa kuliko mtu yeyote hivyo hawezi kuacha kumpenda daima.

No comments:

Post a Comment