Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 30, 2012

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CHAITAKA SERIKALI KUWARUDISHIA VYEO VYAO BAADHI YA WALIMU WALIOVULIWA...!


Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Bw. Gratian Mukoba.

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kimeitaka serikali kuwafutia mashitaka baadhi ya walimu ambao walifunguliwa kwenye mahakama mbalimbali nchini.
Aidha  chama hicho pia kimeitaka serikali kuwarudishia vyeo vyao baadhi ya Walimu waliovuliwa madaraka.
Rais wa CWT Bw. Gratian Mukoba amesema serikali inafahamu fika kuwa Walimu wanaoanza kazi waliongezewa mishahara kwa sh 33, 600, 00 sawa na asilimia 12.12 tofauti na asilimia 14 inayodaiwa kuongezwa.
Vilevile serikali inatambua kuwa Walimu hawakuridhika na hukumu ya Mahakama Kuu ndiyo maana imeamua kukata rufaa, na pia Serikali inatambua kuwa Walimu wanaweza kurudishwa darasani kwa amri ya Mahakama lakini kamwe haiwezi kujituma kufudisha kwa moyo kwa amri ya Mahakama.
Hata hivyo amesema licha ya kuamriwa na Mahakama kukaa meza moja na serikali, lakini Serikali haijawa tayari kukutana na CWT kwa lengo la kujadili mishahara ya Walimu.
Hivyo kitendo cha Serikali kukaa kimya kwa siku 27 bila kufuata agizo la Mahakama ni wazi kwamba ni kukosekana kwa nia njema ya Serikali ya kusikiliza madai yao.

 Chanzo:  Datus Boniface.

No comments:

Post a Comment