Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 21, 2012

Watu wanne wamefariki dunia kufuatia gari walilokuwa wakisafirishia maiti kupinduka...!

Watu wanne wamefariki dunia katika Kijiji cha Mlangali, Chimala katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kufuatia gari walilokuwa wakisafirishia maiti kutoka Jijini Dar es salaam kuelekea Kyela kupinduka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu waliofariki katika ajali ya gari hiyo aina ya Toyota Land Cruiser kuwa ni pamoja na Essau Mwanitete, Lusako Mwakyanjala, Marwa Mokani na Constasia Essau.

Kamanda Athumani amesema kuwa Chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Chimala Mission.
Amewataja majeruhi kuwa ni pamoja na ni Bambombi Mwakyanjala, Atupele Izeck, Tukisigwe Mwakyanjala, Rose Meso, Anyandwile Philipo, Salemu Mwakyanjala na Amosi Mwanitete.

No comments:

Post a Comment