Viongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania Wilaya ya Nzega mkoani Tabora (BAKWATA), wanatarajiwa kufikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha wa zaidi ya Sh bilioni 4.8.
Kesi hiyo kwa sasa inasubiri kupangiwa Jaji kwa ajili ya kuanza kusikiliza malalamiko ya Waislamu ambao kwa kipindi cha miaka saba hawajahi kusomewa mapato na matumizi ya fedha zinazopatikana katika vyanzo mbalimbali vya mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili wa Kikundi cha Wanaharakati wa Kiislamu, Bwana Musa Kwikima amesema kuwa viongozi wanaohusika na tuhuma hizo wapeshapatiwa barua ya kutakiwa kufika mahakamani siku ambayo kesi hiyo itaanza kusikilizwa.
Awali Mwenyekiti wa wanaharakati hao, Shekhe Yusuf Shabani amedai wameamua kuwapeleka viongozi hao mahakamani kutoka na baadhi ya viongozi hao kuhujumu miradi ya Waislamu.
No comments:
Post a Comment