Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni.

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO, DODOMA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kwamba mtu yoyote ambaye anona hakutendewa haki kuhusu kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi anaweza kufafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani.
Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu Pinda wakati akijibu swali la  Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni , Freeman Mbowe lililouliza kuwa Julai 30, mwaka  huu, Serikali ililifungua gazeti la Mwanahalisi  kwa muda usiojulikana kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Maadam katika siku za hivi karibuni serikali imetambua umuhimu wa mahakama ni
Kwanini wamelifungua gazeti hili badala ya kulipeleka mahakamani na wahusika wapate nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa?
 Akijibu swali hilo , Waziri Mkuu Pinda alisema  ni kweli serikali imechukua hatua hiyo, lakini imechukua hatua hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi na “
mtu yoyote kwa msingi wa sheria hiyo anaona hajatendewa haki ni juu yake kutafuta utaratibu mwingine wa  kwenda mahakamani,” alisema Waziri Mkuu Pinda. 
Katika swali lake la nyongeza la kiongozi huyo lililouliza kuwa  Sheria iliyotumika imekuwa ikilalamikiwa na wadau wengi na vyombo vya habari kwa muda mrefu . Je wewe huamini kwa kutumia sheria hiyo ni kunyima haki na ni msisitizo wa utawala usio bora?
 Akijibu swali hilo  Waziri Mkuu Pinda alisema “ Mimi siamini hivyo kwa sababu sheria hiyo imetungwa na Bunge tukufu  na kuwa bado inatumia ni sheria halali, sisi tutaendelea kuitumia mpaka  hapo itakapobadilishwa.