Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 16, 2012

KOFFI OLOMIDE AFIKISHWA MAHAKAMANI BAADA YA KUMPIGA PRODUCER WAKE...!

Koffi Olomide performing in 2005
Koffi Olomide akipiga show kabla ya kudakwa na wama usalama
 
Mwanamuziki mashuhuri wa jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo(DRC) Koffi Charles Antony Olomide amewekwa chini ya ulinzi kwa kosa la kumshambulia mtayarishaji wake wa muziki (Producer).
 
Koffi alitiwa mikononi mwa polisi siku ya jumatano baada ya "Fracas" katika Hotel moja ilioyopo katika mji mkuu wa DRC Kinshansa, Umati wa watu ulifurika katika chumba mahakama kumuona mwanamuziki huyo akipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia Producer wake. Katika kesi hiyo Koffi Olomide anatetewa na mawakili 10.
 
Habari zaidi zinasema Koffi Olomide anamdai Producer huyo kiasi cha Euro 3,000 sawa na dola za kimarekani  3,680 na ni sawa na Paundi za Uingereza 2,345 na ni zaidi ya Shilingi za Kitanzania 5,800,000.
 
Mwanamuziki huyo anaepiga muziki wa dansi kwa staili ya SOUKOUSS neno linalotokana na neno la kifaransa "Secouer" Likimaanisha "Tingisha", Kesi yake iliahirishwa na kama akipatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

No comments:

Post a Comment