Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 12, 2012

ASKARI ANAYETUHUMIWA KUMUUA KWA BOMU DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI MAKALI ...!

Siku Mwanahabari Daudi Mwangosi alivyouwawa kwa bomu.
 
ASKARI, Pacificus Cleophace Simon (23) anayedaiwa kumuua Mwandishi wa Television ya Chanel Ten mkoa wa Iringa, Daudi Mwangosi amefikishwa mahakamani leo
Simon aliyetambuliwa kwa namba G2573 mkazi wa FFU Iringa alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu na waliovaria sare wakiwa na siraha zaidi ya 10.
Pia walitumia gari aina ya Land Cruser (Shangingi) nyeupe yenye namba za usajili T320ARC likisindikizwa na Land Cruser pic up.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama wa wilaya, Dyness Lyimo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mkuu, Michael Luwena alisema inadaiwa kuwa Pacificus Cleophace Simon alitenda kosa hilo Septemba, 2 mwaka huu eneo la Nyololo wilayani Mufindi.
Kesi hiyo ya mauaji imefunguliwa chini ya kifungu 196, kanuni za adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002, Kwa mujibu wa kesi za mada mtuhumiwa hakurusiwa kujibu chochote.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama wa wilaya, Dyness Lyimo alisema mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji hivyo ni kusoma tu.Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 26, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment