Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 12, 2012

GARI YAPATA AJALI NA KUTEKETEA KWA MOTO...!

Huu ni upande wa mbele wa gari iliyoungua moto katika daraja la mto kikavu.

Huu ni upande wa mbele wa ndani (dashboard) ya gari hiyo.

Huu ni upande wa ubavuni wa gari hiyo.

Huu ni upande wa nyuma wa gari hiyo.

Gari aina ya Benzi yenye namba za usajili T432 AHD inayomilikiwa na Thomas Munuo ambaye ni mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali VIAFRICA linalojishuhulisha na kutoa computer katika taasisi za elimu, gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na dereva anayejulikana kwa jina la Mohamed ambaye watu wengi wamezoea kumuita Mood.

Ajali hiyo imetokea leo jioni majira ya saa tisa wakati Mood akitokea Moshi kuelekea Arusha kwenye shuhuli zake lakini kwa bahati mbaya alipovuka daraja la mto kikavu lililopo mkoani Kilimanjaro wilayani Hai gari ilianza kutoa moshi kwenye boneti ndipo dereva huyo alipoamua kuegesha gari pembeni ya barabara ili kuangalia moshi ule ulikuwa ukisababishwa na nini? Kabla hajafungua boneti moto mkubwa ulilipuka na kusababisha gari kuungua moto na hakufanikiwa kuuzima moto ule ambao ulipelekea gari kuteketea yote, lakini kwa bahati nzuri hakuna hata mtu mmoja aliyedhurika kwa ajali hiyo ya moto.

Timu nzima ya www.kingjofa.blogspot.com inawapa pole Thomas na Mohamed kwa ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment