Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, September 14, 2012

CHADEMA WAMBURUZA NAPE KORTINI...!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemfungulia kesi Mahakama Kuu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kutokaa na madai yake kwamba Chadema wanapewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willibroad Slaa, alisema hayo jana wakati wa semina ya viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama wa Chama cha Christian Demokratic Union (CDU) cha Ujerumani.

Semina hiyo kuhusu Uhuru, Demokrasia na Mshikamano  inawashirikisha baadhi ya wabunge na viongozi wa Kamati Kuu ya Chadema ambapo wanajadili masuala ya kukuza  uchumi wa soko unaoshirikisha watu wenye kipato cha chini na juu  ambao unaleta dhana ya uwajibikaji kwa taifa na serikali.

Dk. Slaa alisema Chadema kimemfungulia kesi namba 186 /2012 Nape ili aweze kuthibitisha madai yake kwamba chama hicho kinapata mabilioni ya fedha toka kwa mataifa tajiri.

Alisema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia propaganda ambazo zimekuwa zikielezwa na baadhi ya watu kuwa Chadema wanapata mabilioni ya fedha kutoka nje wakati hakuna ukweli wa suala hilo.

“Ipo propaganda kuwa chadema inapata mabilioni ya fedha toka nje, kimsingi, marafiki zetu kama Konrad Adenauer Stiftung wanatusaidia kwa ajili fedha za kujengea uwezo, lakini siyo kwa ajili ya kuendesha kampeni au shughuli za kiasiasa,” alisema Dk. Slaa.

Chadema hivi karibuni walimtaka Nape kukiomba radhi chama hicho pamoja na kutoa Sh. bilioni tatu, baada ya kudai kuwa Chadema kinapata mabilioni ya fedha toka mataifa ya nje  ambapo alikataa kuomba radhi kwa kueleza tuhuma alizitoa dhidi ya chama hicho ni za kweli.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema mifumo ya uchumi katika nchi yeyote inategemea itikadi na sera ya nchi. lakini serikali ya CCM inaegemea  ujamaa na kujitegemea ilhali sekta za uchumi zipo chini ya soko huria.

Alisema kwa Chadema inafuata mlengo wa katikati ambapo imechukua yale mazuri ya mfumo wa ujamaa na kujitegemea na kuchanganya na sera ambazo zinalenga kumwinua mwananchi kiuchumi. 

Chanzo: Nipashe

No comments:

Post a Comment