Msanii wa kitanzania mwanadada Safina Said Kimbukuta (wa kwanza kushoto) akiwa naa baadhi ya wasanii wenzake kutoka mataifa mbalimbali aliokutana nao Iran.
Msanii wa kitanzania mwanadada Safina Said Kimbukuta amepata bahati ya kwenda kushirikii Tamasha la Sanaa za uchoraji la kimataifa nchini Iran mnamo tarehe 4 September mwaka huu.
Tamasha la 19 la kimataifa la Sanaa la visual ambalo limefanyika katika mji wa Gorgan kaskazini mwa Iran, liliwashirikisha wasanii vijana kutoka mataifa mbalimbali, kukiwa na idadi ya washiriki kutoka nchi kumi na nane ulimwengu, ambalo lilianza tarehe 4 September mpaka 8 September 2012.
Aliporejea alipata wasaa ya kutembelea kituo cha utamaduni cha ubalozi wa Irani jijini Dar as salaam, ifuatayo ni mahojiano aliyoyafanya na jarida la Al-hikma:
Al-hikma: Hii ni Mara yako ya kwanza kutembelea Jamhuri ya Kiislam ya Iran, kiujumla imeichukuliaje safari yako na Taifa hilo la kiislam la Iran?
Safina Kimbukuta: Kwanza napenda kuchukua fursa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kwenda na kurudi salama, kwa kweli ni faraja na fakhari kwangu kupata fursa adhimu kama hii ya kutembelea nchi ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran ni nchi nzuri yenye maendeleo makubwa katika safari yangu nimejifunza mambo mengi na kukutana na  watu kutoka tasnia mbalimbali, kama vile wasanii waandishi wa habari, walimu na wanasiasa.
Al-hikma: Wasanii kutoka Tanzania na Africa walikuwa wangapi na vipi yalikuwa maonyesho?
Safina Kimbukuta: Maonyesho yalikuwa mazuri yaliyokutanisha wasanii mbalimbali ulimwenguni, Kwa upande wa Tanzania nilikuwa Mimi peke yangu na Africa tulikuwa washiriki watatu, Tanzania, Senegal na Zimbabwe.
Al-hikma: Ni kitu gani ulichojifunza na kukuvutia katika Tamasha hilo?
Safina Kimbukuta: Kitu ambacho nilichojifunza na kunivutia ni jinsi ya ustadi wa kazi za wasanii wenzangu ambacho kabla ya hapo nilikuwa sijuwi lakini nashukuru kupitia tamasha lile nimejifunza mengi.
Al-hikma: je kuna kufanana Kwa Sanaa za kazi zako na washiriki wengine na aina ipi ya muundo ulikuwa ukitumia?
Safina Kimbukuta: Kazi za wasanii zilkuwa tofauti, Mimi binafsi nilitumia Metro Structure ambayo ni muundo tofauti na wasanii wengine.
 Al-hikma: Je washiriki wenzio waliichukuliaje kazi za Sanaa yako?
Safina Kimbukuta: wameipokea vizuri kazi yangu japokuwa sikuweza kuzimalizia kutokana na mda kuwa finyu lakini wasanii wenzangu wameonyesha kuvutiwa na kazi zangu.
Al-hikma: Je watanzani wakipata fursa Kama hii unadhani wana weza kuonyesha ushindani wa aina yoyote?
Safina Kimbukuta: Nafikiri watanzania wanao uwezo wakipata fursa kama hizi kushiriki na kuonyesha ustadi wa kazi zao kwa jamii nyingine.
Al-hikma: Umeichukukulisje Iran katakona na mtazamo wa propaganda wa nchi za kimagharibi?
Safina Kimbukuta: Kwanza nilipopata habari juu ya ushiriki wangu wa tamasha la Sanaa nchini Iran, ndugu zangu walishangaa Sana na kuniuliza maswali mengi iweje Iran? Isiwe nchi nyingine, lakini nilivyofika na kukaa mda wa siku tano, mambo Leo yanayozungumzwa na vyombo vya magharibi ni tofauti kabisa na hali halisi iliyopo Iran ni nchi yenye wananchi wenye upendo na amani na nawashauri watanzania wenzangu na kuwaambia kuwa Jamhuri ya Kiislam ya nchi ni yenye ustaarabu  uhuru kamili kwa jamii yoyote na napenda kuwashukuru Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Kiislam wa Iran nchini kwa kufanikisha safari yangu na kurudi salama.