Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, September 14, 2012

DIAMOND ANATARAJIA KUFANYA USAILI WA WATAKAO ONEKANA KWENYE VIDEO YAKE MPYA...!

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia  kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.

“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.

No comments:

Post a Comment