Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 4, 2012

DK. SILAA AMTUMIA IGP SAID MWEMA UJUMBE WA VITISHO...!


Vurugu za CHADEMA mikoani zimechukua sura mpya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk . Wilbrod Slaa, kumtumia ujumbe wa vitisho Mkuu wa Jeshi la polisi(IGP),Said Mwema.
Ujumbe huo uliotumwa kwa njia ya simu ya mkononi unamtaka IGP Mwema kuhakikisha askari wanakuwa na mabomu ya machozi, bunduki na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupambana na wafuasi wa CHADEMA watakaokuwa wakifanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.
Dr Slaa pia amesema iandaliwe karamu ya mauaji, kwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejipanga kukabiliana na polisi wataksokuwa wakiwadhibiti.
Pia amemueleza IGP Mwema na askari wake wajiandae kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.
Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu vurugu zilizotokea juzi, mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel ten, Daudi Mwangosi.
Chagonja alinukuu ujumbe uliotumwa kwa IGP mwema uliosema “Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague”
Akizungumzia ujumbe huo, Chagonja alisema unaonyesha kiburi,ukaidi na kutotii sheria, hivyo jeshi la polisi litachunguza na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa.

No comments:

Post a Comment