Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 4, 2012

MAKETE WAPATIWA MAFUNZO YA SHERIA NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC)...!

Wasaidizi wa kisheria kutoka kwenye kata zilizopo wilayani Makete, wanapatiwa mafunzo ya sheria mbalimbali na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa lengo la kuzidi kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa maeneo hayo
 
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika wilayani hapo kwa kuwakutanisha wasaidizi wote wa kisheria waliopo wilayani hapo kwa lengo la kuzidi kuwajengea uwezo wa kisheria
 
Mkufunzi kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Imelda Urio amewataka wasaidizi hao wa kisheria kuzingatia sheria wanazofundishwa na pia wawe mdsaada mkubwa wa wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria
 
Miongoni mwa sheria walizofundishwa wasaidizi hao hadi hii leo ni pamoja na sheria ya ndoa, sheria ya ajira na mahusiano kazini pamoja na sheria ya ardhi
 
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo, wasaidizi hao wamesema kwa kiasi kikubwa wanapiga hatua na kupata uelewa mkubwa zaidi wa kisheria ambao nao wanautumia kuwapatia msaada wa kisheria wananchi wa maeneo yao
 
“Unajua watanzania wengi hatufahamu sheria na ndio maana matatizo ya kisheria yanapotukumba tunakuwa hatuna la kufanya, mafunzo haya yanatupa mwanga walau wa kujua wapi pa kuanzia hili ni jambo jema sana, na tunaomba kituo cha sheria na haki za binadamu kiendelee kutoa mafunzo haya hata maeneo mengine hapa nchini”alisema msaidizi wa kisheria Nebart Sigala kutoka kata ya Lupila wilayani Makete
 
Mafunzo hayo yaliyoanza jana yanatarajiwa kuhitimishwa hapo kesho

No comments:

Post a Comment