Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 3, 2012

HAYA NDIO ALIYO YAZUNGUMZA FREEMAN MBOWE KUHUSU MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI...!

katiba yetu hii mbovu tuliyonayo inasema wazi, "Uhuru wa Maoni, Sheria ya 2005 Na. 1 ibala ya 5 inasema"
Kila mtu:-
(a)anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

(b)anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi;

(c)anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na

(d)anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Ndg zangu watanzania sheria hii iko wazi kuhusu uhuru wa mtu kufanya kile kilichosemwa kwenye katiba bila kuingiliwa, Nimesikitishwa sana tena sana kwa mauaji wanayoendelea kuyafanya kwa wananchi wa Tanzania wasio na chembe ya hatia, kifo cha Mwandishi Daud Mwangosi kinawaeleza wazi dhamira ya serikali kwa wananchi wake kuwa nikuwauawa wote kama siyo kuwauza. Napenda kuchukua nafasi kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu na marafiki wa marehemu kwa kupotelewa na mpendwa wao aliyekuwa akitafuta haki ya kupata habari, nasema nipo nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi damu yake iwe chachu ya kupinga uonevu na ukandamizaji wa haki za Watanzani unaoongozwa na serikali ya CCM kwa kulitumia jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment