Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 3, 2012

KANISA LATOA TAMKO JUU YA USHOGA...!

VIONGOZI barani Africa hususani nchini Tanzania wametakiwa kuacha
masuala ya kuendekeza ubinafsi,rushwa na kufahamu kuwa yeye
amechaguliwa na wananchi kwa msaada wa Mungu.

Changamoto hiyo imetolewa na mhubiri wa kimataifa kutoka nchini
Marekani Dana Morey wakati akizungumza na waandishi wa habari muda
mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro(KIA) kwa ajili ya mikutano ya injili inayotarajia kuanza
septemba 05 hadi 09 mwaka huu.

Morey amesema tatizo lililopo katika nchi nyingi za afrika ni viongozi
wake kusahau wajibu walioitiwa na kwamba wao kama viongozi ni chombo
ambacho kimewekwa kwa ajili ya kutumiwa na wananchi.


Amesema yeye kama mfanyabiashara wa vipuri vya ndege na magari,anao
wajibu mkubwa wa kumtangaza Mungu na kukemea masuala maovu yakiwemo ya
rushwa kwa mtu wa aina yeyote kutokana na Mungu mwenyewe kuchukizwa na
masuala hayo.

Kuhusu masuala ya ndoa ya jinsia Moja na Ushoga,Muhubiri huyo wa
kimataifa amesema Umoja wa makanisa ya Kipentekoste hauungi mkono hata
kidogo na kutokana na Maandiko kueleza waziwazi,haoni sababu ya yeye
kukinzana na maandiko hayo na ni vyema wachungaji wote nao wakapiga
vita dhambi hiyo.

No comments:

Post a Comment