Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 2, 2012

LUKU zaleta kizaazaa Dar..!

Zoezi la ubadilishaji wa mfumo mpya wa kununua ankara za umeme wa Lipa Umeme Kadri Unavyotumia (Luku) umezua kizazaa jijini Dar es salaam baada ya watu wengi kufurika katika vituo vya kuuzia umeme.

Hivi karibuni Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limetangaza kubadilisha mfumo wa ununuaji umeme wa Luku na kuanzisha mfumo mpya ulioanza kutumika rasmi jana, ambapo wananchi walitakiwa kwenda kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kuingia kwenye mfumo mpya wa ulipaji ankara.

Vituo vilivyotembelewa na Gazeti hili, ilishuhudia misururu mirefu ya wananchi nje ya vituo mbalimbali wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.

Baadhi ya vituo vilivyoonekana kuwa na watu wengi ni pamoja na Magomeni Makanya, Mwenge, Kijitonyama, Ilala, Temeke na katikati ya jiji.

Baadhi ya wananchi waliotakiwa kuelezea zoezi hilo, walisema pamoja na Tanesco kuamua kuanzisha mfumo huo kwa nia ya kuboresha mapato yao, lakini kumekuwepo na upungufu ikiwemo mawakala wengi kutojiandaa na zoezi hilo.

Muhidini Issa mkazi wa Kijitonyama aliyekutwa kituo cha kuuzia umeme cha Oilcom alisema watu wengi wamejikuta wakisimama kwenye foleni kwa muda mrefu wakisubiri kupatiwa huduma kutokana muuzaji wa kituo hicho kufanya kazi taratibu.

"Nilichogundua wauzaji wengi walikuwa hawajajiandaa na zoezi hili kwani wanafanya kazi taratibu sana na kusababisha kuwepo na foleni, angalia mwenyewe jinsi watu walivyojaa hapa kituoni," alisema Issan

Hata hivyo, Muuzaji wa umeme kituo cha Fountain eneo la magomeni Makanya, Twaha ramadhani alisema kiujumla walijiandaa kikamilifu katika zoezi hilo na kwenye kituo chake hakukuwepo na foleni kubwa baada ya kutumia Kompyuta kwa ajili ya kuwahudumia watu badala ya mashine ndogo.

Alisema zoezi la kubadilisha mfumo wa ulipaji unafanyika mara moja kwa mteja kupewa namba za aina tatu ili kufanya Luku yake itambuliwe na mfumo huo na baada ya hapo mteja atanunua umeme kama ilivyo zamani pamoja na kwenye simu zao za mkononi.

No comments:

Post a Comment