Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 2, 2012

Mh. Kikwete ahudhuria mazishi ya Aliyekuwa Waziri wa Ethiopia Melis Zenawi...!


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Septemba Mosi, 2012, ameaga mwili wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi ambaye alifariki dunia usiku wa Agosti 20, mwaka huu.
Rais Kikwete ambaye aliwasili mjini Addis Ababa mchana wa jana
kushiriki mazishi ya Mheshimiwa Meles Zenawi yanayofanyika leo, jumapili, 2 Septemba, 2012. Ameuaga mwili wa Mheshimiwa Meles Zenawi kwenye Kasri ya Waziri Mkuu. Rais Kikwete ambaye msafara wake ni pamoja na Mheshimiwa Salim Ahmed Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu na ambaye kwa miaka 10 alikuwa Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) uliokuwa na makao makuu yake mjini Addis Ababa aliwasili kwenye Kasri ya Waziri Mkuu kiasi cha saa 10 na dakika 35 mchana na kwenda moja kwa moja kutia saini kwenye kitabu cha maombolezo.

Baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo, Rais Kikwete aliweka shada la maua kwenye jeneza la mwili wa Mheshimiwa Meles Zenawi na baadaye akaijulia hali na kuipa pole familia ya Mheshimiwa Meles Zenawi akiwamo mjane wa marehemu, Mama Azeb Mesfin ambaye alipigana msituni pamoja na Mheshimiwa Meles Zenawi na pia ni Mbunge katika Bunge la Ethiopia. Mbali na Mheshimiwa Salim Ahmed Salim, ujumbe wa Tanzania kwenye mazishi ya kiongozi huyo unawashirikisha waliopata kuwa mabalozi wa Tanzania katika Ethiopia Jenerali Sam Hagai Mirisho Sarakikya na Mheshimiwa Christopher Liundi.

Wengine katika msafara huo ni Waziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Haroub Ali Suleiman na wabunge Mheshimiwa
Livingstone Lusinde (CCM-Mtera) na Mheshimiwa Zitto Kabwe (Chadema – Kigoma Kaskazini). Rais Kikwete alimfuatia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Rais Boni Yayi wa Benin na yeye akafuatiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika kuuaga mwili wa Mheshimiwa Meles Zenawi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa kimataifa mara baada ya
kusalimiana na familia ya Mheshimiwa Meles, Rais Kikwete amemwelezea
kiongozi huyo wa Ethiopia kama “mtu mkweli ambaye katika maisha hakusita kusema jambo aliloliamini.” Amesema Rais Kikwete: “Alikuwa kiongozi mwenye uwezo mkubwa. Ucheshi wake, bongo yake, imani yake katika masuala makubwa ya maendeleo ni mambo yasiyokuwa rahisi kuyapata kwa viongozi wengi. Ni bahati mbaya sana amekufa akiwa mdogo”. Mheshimiwa Meles Zenawi amefariki akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuwa ameingia madarakani miaka 21 iliyopita wakati alipokamata madaraka ya urais kufuatia vita ya msituni.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
2 Septemba, 2012

No comments:

Post a Comment