Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, September 6, 2012

MADAKTARI WA HOSPITALI YA MAWENZI WALALAMIKIA UCHAKAVU WA MITAMBO YA KUFANYIA KAZI...1

Madakatari katika hospitali ya mkoa wa kilimanjaro mawenzi wanalazimika kutumia uzoefu kuchunguza maradhi  kwa wagonjwa kutokana na uchakavu wa mitambo katika hospitali hiyo kongwe.
 
mkuu wa kitengo cha X ray katika hospitali hiyo Dr Efraim Minja ametaja baadhi ya mashine ambazo ni mbovu kuwa ni pamoja na X-ray  na Utral Sound ambazo zina uwezo wa kupima hadi wagonjwa 60 kwa siku badala ya uwezo wake halisi wa kupima wagonjwa  150.
 
Dr minja ametoa taarifa hiyo kwa bodi mpya  ya wananchi ya ushauri na usimamizi wa hospitali hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni kufuatia  mabadiliko ya uendeshaji wa hospitali za mikoa ambazo zitasimamiwa na bodi badala ya makatibu tawala wa mikoa .
 
Pamoja na tatizo hilo hospitali hiyo inayotegemewa na wananchi walio wengi imesimamisha huduma za upasuaji baada ya vyumba kadhaa vya upasuaji kufungwa na wizara ya tangu mwaka 2010 kwa madai ya kutokidhi vigezo vya utoaji wa huduma vinavyotakiwa na shirika la afya duniani WHO.
 
Naye mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dr mtumwa Mwako amesema amekuwa akiwasiliana na wizara ya afya mara kwa mara juu ya matengenezo ya mashine hizo.
 
 Bodi hiyo yenye wajumbe kumi na tano ilitembelea hospitali hiyo kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha huduma za afya kama ilivyoainishwa katika mwongozo mpya wa wizara ya afya unaoziweka hospitali za serikali chini ya bodi ili kuongeza ufananizi katika utoaji huduma.
 

No comments:

Post a Comment