Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, September 6, 2012

WANANCHI WA MOSHI VIJIJINI WALALAMIKIA UJENZI MBOVU WA BARABARA...!

Wananchi wa vijiji vya tsuduni, kikarara na kidia kata ya old mashariki wilayani moshi  wameilalamikia halmashauri ya wilaya hiyo kwa kujenga barabara ya kiwango cha moram chini ya kiwango kwa gharama kubwa.

Wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea barabara hiyo wananchi hao wamedai kuwa, ingawa barabara hiyo ambayo imegharimu zaidi ya shs. 26.5mil/= lakini hailingani na thamani halisi ya kazi iliyofanyika.

Baadhi ya wananchi hao Bw Tittus Maro na Bi. Rachel Mshiu wamesema, kiwango kilichotengenezwa barabara hiyo kinahatarisha maisha yao na madaraja na makalvati yaliyojengwa yako chini ya kiwango.

Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wenzake ambao ni wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha tsuduni bw exaud masamu amedai  kuwa hawakushirikishwa katika mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo kinyume cha taratibu.

Hata hivyo mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo injinia joab mutagabwa amesema, moram katika barabara hiyo inawekwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na kazi iliyofanyika ni kuichonga na kuwekwa moramu mita zaidi ya 500 tu.

No comments:

Post a Comment