Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 25, 2012

MAMIA WAJITOKEZA KUSINDIKIZA MGOMBEA UDIWANI KUCHUKUA FOMU...!

Mamia ya wakazi wa kata ya Luwumbu wilayani Makete wamejitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Mchungaji Enock Ngajilo kuchukua fomu ya kugombea kiti hicho

Zoezi hilo lililofanyika katika shule ya msingi Luwumbu zilipo ofisi za msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata hiyo, pia lilitanguliwa na masafara wa pikipiki zenye bendera ya CCM pamoja na msururu wa wakazi wa kata hiyo, huku shughuli za ufundishaji shuleni hapo zikisitishwa kwa muda kutokana na baadhi ya waalimu na wanafunzi kutoka nje kushangaa umati huo

Akikabidhi fomu hizo kwa masimamizi msaidizi wa uchaguzi huo Bw. Asafu Mahenge amemtaka mgombea huyo kusoma kwa makini maelezo ya fomu hizo ili azijaze vyema kuepuka kupoteza sifa za kuwa mgombea pindi atakavyozirejesha

“Ndugu mgombea tafadhali naomba ukasome kwa makini maelezo ya fomu hiyo kisha uzijaze na uzirejeshe kwa wakati na usisite kuwasiliana na ofisi hii mapema kwa msaada zaidi, ofisi ipo wazi katia ya saa mbili hadi saa kumi jioni” alisema Mahenge

Kabla ya kumkabidhi fomu hizo alimtaka mgombea huyo kulipa gharama ya Tsh. 5000/= pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwenye chama chake suala ambalo alilitekeleza hivyo kukabidhiwa rasmi fomu hizo

Amesema pia wao kama wasimamizi wa uchaguzi huo mdogo wamejipanga vyema kuhakikisha zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu linaendelea vizuri hata wakati wa kampeni na uchaguzi huku akisema kuwa hadi leo hii chama cha mapinduzi pekee ndicho kimechukua fomu za kugombea katika uchaguzi huo

Akizungumza na wananchi waliofurika kumsindikiza mgombea huyo kwenye ofisi za CCM kata ya Luwumbu, katibu wa CCM wilaya ya Makete Bw. Miraji Mtaturu amewataka wananchi hao kuendeleza ushirikiano wao na CCM hadi siku ya uchaguzi

Amesema mshikamano waliouonesha tangu mgombea huyo anachukua fomu uendelee kwani lengo la wao kama chama kumteua Ngajilo ni kuleta maendeleo ya kata hiyo na kuendeleza majukumu yaliyoachwa na diwani aliyefariki marehemu Dominiki Tweve

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Jasel Mwamwala amewataka wananchi hao kuziandaa na kuzitunza shahada zao za kupigia kura ili siku hiyo ya uchaguzi kila mtu mwenye vigezo apige kura

Amesema upatikanaji wa diwani mahiri katika kata hiyo utatokana na kura zao huku akisisitiza kuwa anaimani kuwa wananchi hao watamchagua diwani kutoka CCM

Naye mgombea huyo wa CCM Mch. Enock Ngajilo amewashukuru wananchi hao waliomuunga mkono wakati wa uchukuzi fomu na kusema kuwa jambo hilo limempa imani kuwa yeye ndiye ataibuka mashindi katika uchaguzi huo

“Ndugu zangu nimetumika sana katika maeneo mbalimbali nchini ila kwa sasa nimeamua nije kutumikia kata hii ambayo ni asili yetu, tuwe pamoja hadi mwisho wa mchakato huu, kwani maendeleo haya ya kata hii ya Luwumbu yataletwa na CCM” alisema Ngajilo

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Marehemu Dominiki Tweve aliyefariki Februari mwaka huu

No comments:

Post a Comment