Tarehe 23, august 2012 nilipost habari ya ajali mbaya iliyotokea eneo la ilala boma na kijana mmoja ambaye kwa wakati huo hatukuweza kupata jina lake aligongwa na kupasuliwa kichwa na lori na dereva wa lori hilo kukimbia. Mpaka wakati napost habari hiyo hatukuwa tumepata majina kamili ya kijana huyo aliyegongwa wala dereva. Huyo mtoto aliyegongwa anaitwa ABDULKARIM MOHAMED MDEE, alikuwa na miaka 11 mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi ILALA BOMA....baada ya kumgonga dereva wa roli alikimbia na kujisalimisha polisi na kesi yake imetajwa tarehe 3-9-2012 ambapo amehukumiwa kulipa faini ya fedha za Kitanzania shilingi 50,000 au jela miezi 6. Shukrani za kipekee zikufikie popote ulipo Zennat Khamis.
Je adhabu aliyopewa dereva huyo inalingana na kosa alilolifanya?
Je adhabu aliyopewa dereva huyo inalingana na kosa alilolifanya?
Baadhi ya wananchi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza maisha papo hapo mara baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na hatimaye kupelekea kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la ilala boma
Mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ukiwa umefunikwa na kanga huku pembeni vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni mara baada ya kugongwa na lori na kukanyangwa kichwa na kupelekea kichwa kupasuka na ubongo wote kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la Ilala Boma. Kijana huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Msimbazi.
Askari wa Usalama barabarani akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ili kuupakia katika gari dogo tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana huyu anakadiriwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Msimbazi.
Baadhi ya wananchi wakiutazama mwili wa marehemu ambaye amegongwa na gari na kupelekea kupasuka kichwa na kupoteza maisha papo hapo.
No comments:
Post a Comment