Mawaziri sita wa muungano tawala nchini India wamejiuzulu, kufuatia mipango ya serikali ya kuruhusu maduka makubwa ya kigeni kuendesha sekta ya bidhaa za reja reja nchini humo.
Duru
zinaarifu kuwa uamuzi wa chama cha Trinamool Congress kikiongozwa na
Mamata Banerjee,kutounga mkono muungano huo zinazidisha shinikizo za
kisiasa ingawa hazitishii ushawishi wa chama cha serikali.
Waziri mkuu
wa nchi hiyo, Manmohan Singh, anatarajiwa kutoa taarifa kupitia
televisheni ya kitaifa kutetea sera zake kuhusu uwekezaji wa kigeni na
kuondoa ruzuku ya mafuta.
Chanzo - BBC Swahili
No comments:
Post a Comment