Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 18, 2012

MWANAMKE AJIFUNGUA KIUMBE WA AJABU MBEYA ...!

Kichwa cha ng'ombe.
Kiwiliwili cha binadamu.

Mwanamke Shija Paulo(35),mkazi wa Kijiji cha Magaga,Kata ya Mbuyuni Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amejifungua kiumbe kinachofanana na ng'ombe chenye jinsi ya kiume.

Mwanamke huyo alijifungua Septemba 16 mwaka huu majira ya saa 11 alfajiri.
 
Imeelezwa kwamba alipopelekwa katika Zahanati ya Mbuyuni kwa ajili ya kujifungua akiwa na mumewe Mwigulu Yangula(Makeni) lakini kabla ya kufika zahanati mwanamke huyo alipatwa na uchungu ndipo alipoomba msaada kwa Mkunga wa jadi aliyekuwa karibu Bi. Agripina Fredrick Sikanyika(Namwinje).

Mkunga huyo alimpokea na kujifungua salama huku kiumbe hicho kikiwa na kichwa na mdomo mithili ya ndama(mtoto wa ng'ombe) chenye dalili ya kuota mapembe na manyoya meusi hadi eneo la kifuani ambapo kutoka hapo kifuani mpaka miguuni alikuwa na umbile la binadamu na jinsi ya kiume  licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa na uzito wa wastani.

Hali hiyo imeelezwa kuwa ilimtia hofu Mkunga Sikanyika na kuitwa Bwana Yangula kushuhudia kiumbe hicho naye alistaajabu kwa yale yaliyotokea.

Hata hivyo kiumbe hicho kilidumu kwa muda wa masaa  matatu na kufariki dunia ambapo uzazi huo kwa mwanamke huyo ulikuwa ni wa mimba ya nane na kila mimba hupata watoto ambao si riziki.

Tukio hilo pia lilishuhudiwa na mhudumu wa Kituo cha Afya,kitongoji cha Magaga Josephat Alisen Ismail,ambaye naye amesema ameshangazwa na tukio hilo na kusema hajawahi kukutana na jambo hilo katika taaluma hiyo ya utabibu.

Wakati wa tukio hilo Afisa Mtendaji wa Kijiji Michael Sanziwa hakuwepo na alipopigiwa simu aliruhusu kiumbe hicho kichukuliwe na mzazi ambapo maziko yake yalifanyika kandokando ya nyumba ya Bwana Yangula.

Katika tukio hilo watu wengine wamelihusisha na imani za kishirikina na wataalamu wa viumbe wamesema kuwa mara nyingi viumbe hivyo huwa haviishi muda mrefu,lakini hali ya mama aliyejifungua inaendelea vema baada ya kujifungua.
 
 
  Na Ezekiel Kamanga

No comments:

Post a Comment