Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 27, 2012

Madarasa ya Shule ya Ufundi Moshi yageuka kuwa Magofu...!

Kijana akipiga mswaki eneo la shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
 
SHULE ya Sekondari ya Ufundi Moshi iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani  Kilimanjaro ni miongoni mwa shule za Serikali iliyokuwa ikifanya vizuri kwa kutoa wasomi wengi miongoni wapo serikalini na taasisi binafsi.
Ilianzishwa  mwaka 1957 ikiwa kama shule ya masomo ya biashara na ilipofikia mwaka 1967 ilibadilishwa na kuwa shule ya sekondari ya ufundi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Kwenye miaka ya 1970 na 1980, ilikuwa na mazingira nadhifu kwa kuwa na majengo ya mabweni na vyumba vizuri vya kusomea. hali hiyo pia ilikuwa ikiandamana na matokeo mazuri kwa wanafunzi wengi.

Leo hii ukichunguza mazingira yake yalivyo ukalinganisha na hali na hadhi iliyokuwa nayo miaka 30 iliyopita waweza kupata wazo ambalo linawiana na msemo wa Kiswahili usemao: "Ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka."

Sasa iko katika hali mbaya kiasi kwamba hata wanafunzi hawawezi kuingia msalani kutokana na miundombinu ya shule hiyo kuwa mibovu kupita kiasi.

Leo hii wanafunzi waalazimika kutumia choo kilichojenga mwaka juzi kwa ajili ya walemavu chenye matundu  matatu ambacho kinatumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo anasema vyoo na bafu vilijengwa tangu shule ilipoanzishwa na vimekuwa havifanyiwi ukarabati wala kujengwa vipya jambo ambalo limesababisha kuchakaa kiasi kwamba havifai kutumika.

Ukiingia baadhi utaona kuta zimoka sakavu imeharibika na vingi vinatiririsha maji machafu pembeni nu kusababisha vigeuke kuwa mazalia ya nzi, mende na wadudu wengine wanaotambaa.

Anasema wanafunzi wanashindwa kuvitumia vyoo hivyo mchana na mara nyingine wanajikuta wakilazimika kwenda kijisaidia kwenye vichaka  karibu na shule hiyo.

Kutokuwa na maeneo ya kujisetiri faraga wakati wa kuoga, kumekuwa kukiwafanya wasubiri usiku wa giza ambao siyo rahisi kuonekana wao kwa wao au wapitanjia.

Alisema kufuatia uchakavu wa majengo, baadhi ya mabati yaliyoezekea majengo hayo yametoboka na wakati wa mvua yanavuja na hata kusababisha dari kuchakaa na mara kadhaa vipande vyake vimekuwa vikiwadondokea.

“Yaani  hii shule iko katika hali mbaya kiasi kwamba hata sisi tunaosoma hapa tunaona tuko kama tunasomeshwa bure kumbe tunalipa ada na wazazi wanajua tuko katika shule nzuri. Kumbe mazingira haya ni mabaya," anasema mawafunzi huyo.

Uchakavu wa shule hiyo ipo hadi kwenye miundo mbinu ya usambazaji wa umeme na sasa majengo mengi hayana umeme jambo linalowalazimisha wanafunzi kutumia mishumaa wakati wa kusoma.

Licha ya uchakavu huo, wanafunzi wanalalamika kwamba wanafunzi wanaosajiliwa kila mwaka ni wengi kuliko uwezo wake.

“Kwa kweli! Kiwango cha elimu  hapa shuleni kinashuka kutokana na mfumo wa shule ulivyo waalimu hawajali ni sawa na kwamba hawathamini kazi zao na mazingira wanayofanyia," anasema mmoja.

Anatoa mfano wa darasa lake kuwa lina wanafunsi zaidi ya 100 wakati uwezo wake halisi ni kati ya 45 hadi 50.

Anasema wakati mwalimu anafundisha, baadhi ya wanafunzi hushindwa kuingia darasani na kubakia kusikiliza wakiwa nje jambo ambalo linapunguza usikivu wa umakini.

“Wanafunzi wengi hawaingii darasani kwa kuwa unakuta hakuna sehemu ya kukaa wakiingia wengine wanakuwa wanazunguka tu na wala walimu hawasemi chochote,” analalamika mwanafunzi huyo.

Tatizo jingine ni shule hiyo kutokuwa na vifaa vya kufundishia wanafunzi walemavu, jambo ambalo linawapa shida kuendana na mazingira halisi ya ufundishaji hivyo kushindwa kupata elimu iliyokusudiwa.

Wanafunzi hao walisema walemavu walioko shuleni hapo hawatendewi haki kwa kuwa wanachanganywa na wanafunzi wakawaida bila kujali ni mlemavu wa aina gani.

“Hapa shuleni tuna walemavu ambao hawana uwezo wa kusikia sauti na wengine wasioona na vipofu na huwa tunachanganywa nao madarasani hawana waalimu wa kuwafundisha na unakuta hata hawaelewi chochote.” alisema.

Alisema baadhi ya waalimu  hawaingii kufundisha darasani na pale wakijisikia na pale tunapohoji  wanafunzi wanafukuzwa shule  kwa kuwa hivi karibuni kuna baadhi ya viranja pamoja na wanafunzi ambao walihoji kuhusu ufundishaji  na wote walifukuzwa.

Alisema wanafunzi wengi wamekuwa wanahofia kuzungumza hadharani matatizo ya shule hiyo kwa hofu ya kufukuzwa shule.

“Pamoja na ubovu wa vyoo, madarasa na mabafu hatuthubutu kulalamika kwa kuwa hofu ni kupatiwa barua ya kufukuzwa shule,” alilalamika.

Anadai kuna wanafunzi waliwahi kufukuzwa shule kutokana na kitendo cha kuhoji ratibu ya vyakula kwa sababu wanafunzi wamekuwa wakipikiwa Ugaki na maharage kila siku.

Anasema  wanahofia maisha yao wakati wakiwa wamelala kutokana na bweni la wasichana  kubomoka na wote kuhamia gorofa ya kwanza ambapo wanalazimika kulaa wanafunzi wanane hadi 10 katika chumba kimoja ambacho kina uwezo wa kulaza wanafunzi wanne.

Anaema gorofa ya juu ya jengo wanalolala limebomoka na hata ngazi zimevunjika kiasi kwamba ni hatari katika maisha yao.


“Tumelalamika kwenye uongozi wa mara kadhaa bila mafanikio,: lialaliachochote na ndio shule tuliopangiwa tukifikiria wengine wazazi wetu hawana uwezo wa kutuhamisha kwenda shle nyingine inatubidi  tuvumilie shida hizi,” anasema.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Maddy Kisuu, alikiri shule hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, miundo mbinu na kushuka kiwango cha taaluma.

Kisuu anasema hali hiyo imechangiwa na Serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo huko miundombinu ya majengo ikiwa ni ile ile.

Anasema shule hiyo yenye wanafunzi  1,476 ina waalimu 17 na kusababisha kiwango cha elimu kushuka kupita kiasi kutokana na upungufu wa walimu.

Mkuu huyo anasema  shule hiyo pia ina wanafunzi wenye matatizo ya kusikia 100 lakini ina walimu 5 kwa ajili yao jambo ambalo halitoshelezi kukidhi matakwa yao kikamilifu.
Anasema shule hiyo ni miongoni mwa zile zilizokuwa zikitoa wataalamu mbalimbali wa ufundi nchini lakini kwa sasa kiwango cha elimu kimeshuka kutokana na kukoza mazoezi kwa vitendo.

Katika kuthitisha hilo, anasema rekodi ya matokeo ya mithani wa kidato cha nne mwake 2007 yanaonyesha wanafunzi waliofaulu kwa daraja la kwanza 60 kati wanafunzi 230. Katika mwaka 2009 wanafunzi 14 tu kati ya 117 ndio waliofauli daraja la kwanza na na mwaka 2011 wanafunzi 29 kati ya 153 ndio walofaulu kwa daraja la kwanza.

Kwa matokeo ya kidato cha sita  2006 /2007 wanafunzi saba kati ya 152 ndio walifaulu kwa daraja la kwanza na  2007 /2008 hakukua na aliyefaulu kwa daraja la kwanza kati ya wanafunzi 101 na mwaka 2010/2011
 waliofaulu kwa daraja la kwanza walikuwa tisa kati ya  151 na 2011/2012 wanafunzi wawili kati ya 183 ndio walifaulu kwa daraja la kwanza.

Kwa upande wa walemavu, hakuna aliyeweza kufaulu kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita.

Chanzo: Fina Lyimo, Moshi

No comments:

Post a Comment