Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, September 10, 2012

Pinda ziarani Mwanza wiki nzima

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kesho anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya wiki nzima mkoani Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine ataweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo katika wilaya zote nane za mkoa huu.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo amewaambia waandishi wa habari jijini hapa kuwa ziara ya Pinda itaanzia wilaya ya Sengerema ambako ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la samaki katika ufukwe wa Nyakarilo.

Aidha, alisema akiwa wilayani humo, Pinda atakagua shamba darasa la ufugaji nyuki kabla ya kuzindua mradi wa ufugaji wa nyuki kimkoa katika hafla itakayofanyika kwenye viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Sengerema.

Kwa mujibu wa Ndikilo, baadaye Waziri Mkuu ataelekea wilayani Ukerewe ambako atapokea taarifa ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa serikali kuu, kisha ataweka mawe ya msingi katika mradi huo na ule wa ujenzi wa maabara ya kisasa katika hospitali ya wilaya hiyo.

“Akiwa wilayani Ukerewe, Waziri Mkuu pia atajionea banda la mfano bora wa ufugaji nyuki wilayani humo na atahutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mongella mjini Nansio, kisha ataelekea wilayani Magu,” alisema Ndikilo.

Alibainisha kwamba akiwa wilayani Magu, Waziri Pinda atapokea taarifa ya wilaya pamoja na utekelezaji wa mradi wa kilimo cha matunda na mbogamboga (Ngongoseke Horticulture Farm) katika kijiji cha Nsola kwa Ngongoseke.

No comments:

Post a Comment