Wamachinga zaidi ya mia mbili katika eneo la soko la kilombero mkoani Arusha walivamia eneo lililokuwa na uzio na kuvunjwa uzio huo na kuingia katika eneo hilo na kung'oa mabati na miti iliyokuwepo katika eneo hilo na kucanza kuchoma moto. Kwa maelezo ya wamachinga hao wanadai kwamba lilikuwa ni eneo la wazi kwa muda
mrefu lakini baadaye eneo hilo likauzwa na madiwani bila kushirikisha
serikali ya mtaa, kesi ikapelekwa mahakamani na ayeuziwa eneo hilo
akasimamishwa kujenga na kesi ipo mahakamani, Jana
asubuhi wafabiashara ndondogo maarufu kama wamachinga waliamua kuvunja uzio wa eneo hilo na
kujigawia eneo hilo na polisi walikuja wakawa wanaangalia tuu baada ya kuona wingi wa wamachinga hao. Lakini baadae askari waliongezeka na kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kuwasambaratisaha wamachinga hao....
Hali inavyoonekana kwa sasa Eneo la kilombero jijini arusha wananchi waamua kuchoma matairi
Wabomoa uzio wa eneo hilo lililokuwa limezungushiwa mabati
Fire wamesha fika kwa ajili ya kudhibiti madhara yoyote ya moto
Polisi wakiwa eneo la tukio
Sasa Yamekuwa matatu na yote yamejaa FFU kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi..
Chanzo: ujanatz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment