Afisa mtendaji wa kijiji cha kondeni Stella K. Massawe (Kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha kondeni Bw. Lyimo (Kulia). Wakiwa kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya kijiji cha Kondeni
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika kikao cha kujadili maendeleo ya kijiji cha Kondeni
Uongozi wa kijiji cha kondeni kilichopo katika kata ya Mwika
kusini, jimbo la Vunjo umejikuta katika utata ambao mpaka sasa hawajajua
hatima yao kwa kile wanachokilalamikia kuwa ni utendaji mbovu wa diwani wa
kata hiyo. Mtafuru huo ambao unasemekana ni wa muda mrefu ila siku za karibuni
ulionekana kufikia hatua mbaya pale alipokuja mkandarasi wa
barabara ya kutoka kilacha mpaka msae ambayo ni barabara yenye takribani kilometa ishirini
lakini mpaka sasa barabara hiyo imetengenezwa kutokea kwa betueli mpaka msae
ambayo ni takribani kilometa mbili tu na mkandarasi huyo tayari amesha chukua
vifaa vyake katika eneo hilo kitendo ambacho kinaashiria kuwa ameshamaliza kazi hiyo na utengenezaji wa barabara hiyo. Na toka achukue vifaa hivyo tayari umeshapita muda wa wiki mbili. Watendaji hao walikuwa wakitupa lawama kwa diwani kwa kusema walimuona diwani wao akiwa na mkandarasi
wa barabara hiyo lakini hawajui ni nini kinachoendelea kati ya mkandarasi huyo na diwani.
Walizidi kulalamika kwa kusema ni rahisi sana kwa viongozi
walioteuliwa na wananchi kula rushwa kuliko watendaji ambao wameajiriwa na
serikali. Pia waliendelea kulalamikia barabara hiyo kuwa haikutengenezwa kwa
kiwango kinachotakiwa. Watendaji hao wanalalamika wakisema wanashindwa kufanya
kazi na diwani kwa kuwa wana tofauti za hitikadi za vyama kwa kusema kuwa
diwani huyo ni kutoka chama cha CHADEMA lakini watendaji hao ni kutoka CCM kwa
maana hiyo wanashindwa kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta maendeleo katika kijiji chao na ndio sababu ameweza
kusaini mikataba na mkandarasi wa barabara bila kuwashirikisha
watendaji wa kijiji. Pia waliendelea kueleza kuwa wamekuwa wakizuia ukataji wa
miti katika katika kata hiyo lakini diwani amekuwa akiwaruhusu wanakijiji kukata miti
katika kijiji anachoishi lakini kwa vijiji vingine haviruhusiwi kukata miti.
King Jofa akifanya mahojiano na Diwani wa kata ya Mwika Kusini Charles Kawiche.
Nilimtafuta
Diwani wa kata hiyo ya Mwika kusini ili kuweza kufahamu zaidi kuhusu tuhuma
dhidi yake. Nilifanikiwa kumpata na Diwani huyo na alinieleza haya “Mimi naitwa Charles
Kawiche ni Diwani wa kata ya Mwika mashariki na pia ni Mwenyekiti wa kijiji cha
kitongare, kero kubwa katika kata hii ni tatizo la maji, kata ya kaskazini kuna
maji na nikafuatilia ili angalau tupate hata maji kwa masaa mawili kwa siku
lakini imeshindikana, lakini kwenye kikao na mbunge Mh. Lyatonga Mrema lakini
pia mpaka sasa hatujapata muafaka wa maji. Kwa swala la barabara tayari nimelifuatilia
na kwa taarifa ya mwisho ni kwamba mkandarasi anatakiwa kuja kurudia
kutengeneza barabara upya ila kwa kuwa watendaji wangu wana haraka na hawajui
ni nini kinaendelea ndio maana wanalalamika na wakati hawajui lolote. Swala la
ukataji wa miti kwa hapa kwenye kata ni kweli ila huwa wanakata miti wakajua mimi nimeenda kwenye vikao, ila wakijua nipo hawakati miti na tayari nimeshashika chenso mbili
zilizokuwa zinakata miti na kuzipeleka ofisini. Kuhusu tofauti za hitikadi za
vyama ni kweli lakini mimi nilishawaeleza kuwa mimi nafanya kazi na yeyote
aliyetayari kufanya kazi bila kujali hitikadi za vyama." Hayo ndio aliyoyaeleza Diwani.
Swali la kujiuliza ni je nani mkweli kati ya Diwani na Watendaji wa kijiji???
No comments:
Post a Comment