Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 5, 2012

WANANCHI TARIME WASEMA POLISI NAO NI ITRUDA...!

Wananchi wa Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara  wamelaani kitendo cha polisi kupiga kwa mabomu na risasi za moto  wananchi maarufu kama intruda katika mgodi  wa North Mara Barrick   na kwamba hawapaswi kufanya mauwaji kwakuwa nao ni miongoni kati ya polisi wanaojihusisha na uintruda.
 
Wakiongea kwa nyakati tofauti na gazeti hili walisema kuwa mbali na wananchi kudaiwa  kuvamia mgodi wapo pia polisi ambao uiba mawe ya dhahabu ndani ya mgodi huo kisha kuuza mawe ya dhahabu  kwa wananchi na kupatiwa fedha.
 
Chacha Mwita mkazi wa Nyangoto alisema kuwa  kitendo cha wananchi kuingia mgodini ni baada ya kupatiwa taarifa na askari polisi wanaolinda mgodi mara tu dhahabu inapoonekana ambapo wananchi uwapatia pesa nakuwaruhusu kuingia mgodini ambapo hata hivyo wananchi hao uungana na baadhi ya polisi kuingia ndani ya mashimo ya dhahabu na kuchukuwa mawe yenye dhahabu.
 
“Nashangaa polisi wanawauwa wananchi nawakati wao ndiyo chanzo  polisi ndiyo wanaosuka mipango yaani mchongo wanawaomba pesa wananchi kisha wanaingia kwenye mashimo  wakiona hali ya usalama ni mbaya au gari la mzungu linapita wanapiga watu mabomu na risasi kuonyesha kuwa wananchi wamevamia mgodi polisi ndiyo wanalinda mgodi na ndiyo wanaojua kuwa mahali Fulani wamemwaga mawe ya dhahabu”alisema Mwita.
 
Mwananchi mwingine ambaye hakutaka jina lake litajewe alisema chanzo cha uvamizi wa mgodi kinatokana na mitandao ya polisi ndani ya mgodi ambao wapo kwa ajili yakulinda lakini lengo lao ni  kuchukuwa mawe yenye dhahabu nakuyaunza kwa wananchi.
 
“Polisi wanaiba dhahabu hivi karibuni kuna polisi  walichukuwa mawe ya dhahabu wakawauzia wananchi wakapata mamilioni ya fedha tunajua na tunawafahamu kwasababu mawe ya dhahabu yanauziwa hapahapa Nyamongo tena pesa hizo wanazitumia kwa starehe wanaita funga baa wananunua creti za bia wanafanya mashindano ya kunywa bia,wakiwabaini wananchi wana mawe ya dhahabu wanawanyang’anya kisha wanawatafuta wateja wao na kuwauzia ni kutu cha wazi na kinafahamika hakuna asiyejua’alisema,
 
Hata hivyo vyanzo vya habari  vingine vina sema kuwa mauwaji ya watu wawili yaliyotokea wiki iliyopita katika mgodi wa Nyamongo inadaiwa kuwa ilikuwa ni plani ya polisi ambao baadhi yao namba zao za simu tunazo akiwemo askari aliyedaiwa kujeruhiwa na intruda  siku ya mauwajiya wananchi ambapo RPC Justus Kamugisha alisema kuwa  askari mmoja   No. E 6059 D/CPL Julius alijeruhiwa na maintuda kwa kukatwa panga usoni na kupata majeraha mdomoni na mgongoni.
 
Ambapo kwa maelezo ya vyanzo vya habari wanasema siku ya mauwaji askari huyo Julias akiwa na askari aliyefahamikwa kwa jina moja Kimaro wa Musoma ambaye  yuko rikizo kwa matibabu lakini yuko Nyamongo akijihusisha na uintruda waliingia ndani ya shimo la dhahabu maarufu kama piti 

Polisi hao wanadaiwa kuwa walichukuwa mawe ya dhahabu ambapoa hata hivyo kutokana na intruda kuwa wengi walipata hofu na hivyo kuwatawanya kwa mabomu na risasi na hivyo kusababisha vifo vya watu 2 na majeruhi mmoja ambapo pia wananchi nao waliweweza kumjeruhi kwa mawe askari Julias.
 
Hata hivyo Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alipohojiwa kujua kama anataarifa ya madai ya polisi wake kujiusisha na wizi wa mawe ya dhahabu mgodini hapo licha ya kuwa ni walinzi wa mgodi hakuwa tayali kusema chochote  badala yake alimtaka mwandishi amsaidie kufanya uchunguzi ambapo pia alisema hataki kuona mwandishi wa habari ofisini kwake kwa madai kuwa wanatoa tarifa za uongo.

NB. namba za askari hao ni
 0784274196 ni ya askari Kimaro na 0784728477 anaitwa Julias askari hao ni maarufu wa kuiba mawe mgodini na kuuza kwa watu.

No comments:

Post a Comment