Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 5, 2012

HALMASHAURI YAWEKA MIKAKATI MATHUBUTI YA KUKUSANYA MAPATO...!

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara wameitaka Halmashauri hiyo kutafuta wataalamu kutafiti namna ya kupata vyanzo vya mapato ili iweze kukua kimapato badala ya kusubiri ruzuku kutoka Serikalini.

Wakiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani. Madiwani hao walisema kuwa Wilaya ya Rorya ina vyanzo vingi vya mapato lakini pato linalopatikana haliendani na vyanzo vilivyopo jambo linalosababisha kutoongezeka kwa pato la ndani la halmashauri na badala yake kungoja pesa za ruzuku ya Serikali kutekeleza mahitaji ambapo ruzuku hiyo haitoshelezi.

Diwani wa kata ya Kisumwa Piter Malaki (NCCR) amesema kuwa Pato la Halmashauri halikuwi licha yakuwa kuna vyanzo vingi  na hivyo kuoba watafutwe wataalamu watakaopitia na kufanya utafiti wa kujua na kupata vyanzo  vya ndani vya mapato badala ya kungoja ruzuku kutoka Serikalini ambayo haifiki kwa wakati.

Diwani wa Tarafa ya Nyancha Pendo Odelle( CCM) amesema usimamizi mbovu wa mapato ya ndani ndiyo uchangia kutoongezeka kwa pato kwani halmashauri imeshindwa kufatilia na kujua  namna ya ukusanyaji mapato unavyofanyika hususani kwa mawakala wanaokusanya ushuru kwa madai kuwa kuna mawakala wamekuwa wandanganyifu ambapo ukusanya pesa nyingi huku halmashauri ikipata pato kidogo.

Diwani wa kata ya ya Kitembe Thomas Patrick(CHADEMA) amesema bila kusimamia mapato ya ndani halmashauri haiwezi kusonga  kwa madai kuwa soko la Obwele lililoko Shirati limekuwa likipoteza mapato mengi kutoka na na uzembe wa ukusanyaji mapato kutokana na wakusanyajiushuru kukaa kando na kungoja wafanya biashara wawapelekee pesa ya ushuru ambapo wengine uondoka bila kulipaushuru.
Diwani wa kata ya Ikoma Laulent Adriano(CCM) amesema kuwa tatizo ni halmashauri kutotoa viwango halisi vya ushuru wa bidhaa zinazotozwa kwakuwa kuna watendaji wa kata na vijiji wamekuwa wakitoza wananchi  viwango vikubwa isivyo halali  na kuwafanya kukwepa ushuru.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Rorya Andreas Madundo amesema kuwa inawezekana kufanya utafiti wa kina wa vyanzo vya mapato lakini kufikia lengo itakuwa  ni juhudi za ziada kwa madai kuwa tangu kustishwa kwa ruzuku za fidia kumechsangia halmashauri kutofikia malengo yake kwani makusanyo yanayopatikana ni kidogo ukilinganisha na vyanzo vichache vya mapato vilivyoko ndani ya halmashauri hiyo.

Halamshauri ya Rorya kwa kipindi cha Julai 2011- juni 2012 vyanzo vya halmashauri makisio  2011/2012 ni 1,491,977,00.00,makusanyo julai 2011-mei 2012 ni 573,  104,098.00,makusanyo juni 2012 ni 22,105,637.00 ambapo jumla ya mapato kutoka julai 2011 –juni 2012 ni 595,209,735.00 sawa na asilimia 40%.

Wakati huo huo,
MKUU wa Wilaya ya Rorya Elias Goroi ameahidi kusimamia mapato ya halmashauri ya wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha  fedha za miradi zinazotolewa inatekelezwa kwa wakati.

DC Goroi alisema kuwa mapato ya halmashauri yanapaswa kuongezeka  na siyo kila mwaka  mkaguzi anakuta mapungufu na kuwa kwa wale watakao bainika katika matumizi mabaya  ya fedha  watachukuliwa hatua za kisheria

Aliongeza kuwa Halmashauri inapaswa  kuhakikisha pesa zinazotolewa zinatumika vizuri na kwamba nidahamu itumike katika ukusanyanji wa mapato wilayani Rorya kwakuwa pesa hizo ni za wananchi.

No comments:

Post a Comment