Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 25, 2012

WAREMBO WALIPATA NAFASI YA KUSHIRIKI MISS TANZANIA...!

Redds Miss Lake zone 2012/13 Eugene Fabian (katikati) akiwa pamoja na , mshindi wa Tatu Happiness Rweyemamu na Kulia kwake ni mshindi wa pili Happiness Daniel warembo hawa wataingia kambi ya REDDS Miss Tanzania 2012.

Redds Miss kanda ya Kaskazini Warida Frenk katikati akiwa na washindi wenzake Anande Raziel kulia na lucy stefano kushoto mara baada ya kutawazwa kuwa washindi wa Redds Miss Kanda ya kaskazini,Washindi hao wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya Redds Miss Tanzania hapo baadae ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds Miss Tanzania.

Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1, mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.

Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irine akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.

Malkia wa Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester (katikati), akiwa na mshindi wa pili Flavian Maeda (kushoto), pamoja na Catherine Masumbigana aliyeshika nafasi ya tatu katika kilele cha mashindano hayo, Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

 Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward


Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo (katikati) akiwa na mshindi wa pili Lightness Michael (kushoto) na mrembo aliyetwaa nafasi ya tatu Elizabeth Diamond baada ya kumalizika kwa shindano hilo mjini Dodoma hivi karibuni. warembo hawa wote wameingia kambi ya Miss Tanzania 2012.


Redds Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalena Munisi (kulia) na mshindi wa tatu Mary Chizi (kushoto) mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Ilala 2012.

Chanzo: www.mrokim.blogspot.com

No comments:

Post a Comment