WASIMAMIZI 369 Wilayani Tarime Mkoani Mara wanaotarajia kusimamia mitihani ya wanafunzi wa darasa la saba itakayoanza jumatano na Alhamisi ya wiki hii wametakiwa kusimamia mitihani kwa kuzingatia taratibu za uendeshaji mtihani na kwamba kwa yeyete atakayeenda kinyume au kubainika kuonyesha wanafunzi majibu atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akiongea na V.FM ofisini kwakwe Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tarime Emanuel Jonson amesema kuwa endapo wasimamizi wa mitihani wakisimamia vyema itasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi ambao wamekuwa wakifutiwa mitihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kuonyeshwa na kuonyeshana majibu.
Jonson amesema kuwa katika mtihani wa mwaka jana kwa shule za Serikali jumla ya wanafunzi 59 kati yao wavulana 22 na wasichana 37 walifutiwa mtihani wa darasa la saba huku wanafunzi wa shule Binafsi 63,wavulana 34 na wasichana 29 nao walifutiwa na kwamba wote wanatarajia kurudia mtihani huo utakaoanza siku ya jumatano.
Jonson amesema kuwa Wilaya ya Tarime ina jumla ya shule za mshingi 128 ambapo shule za Serikali ni 121 binafsi 7 Nakwamba jumla ya watahiniwa wote wa shule za Serikali na binafsi zipatazo 128 kwa Wilaya nzima watahiniwa wapatao 8146 wavulana wakiwa 4001 na wasichana 4145 watafanya mtihani.
No comments:
Post a Comment